Mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Sikukuu ya Wafanyakazi Mei Mosi 2022, Mkuu wa Wilaya ya Mlele Mh.Filberto Sanga(Aliyevalia Suti Katikati) kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi akipokea maelezo kuhusu namna ya kurekebisha Mfumo wa Gurudumu za Gari kwa kutumia Mfumo wa Kompyuta kutoka kwa Mkufunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi VETA-Mpanda alipotembelea Banda la maonyesho katika maadhimisho ya Sikukuu ya Wafanyakazi Mei Mosi 2022 yaliyofanyika katika Uwanja wa Kashaulili Manispaa ya Mpanda.
Na: John Mganga-IO-Katavi RS
Wafanyakazi kutoka Taasisi mbalimbali za Umma yakiwemo mashirika pamoja na Taasisi Binafsi Mkoani Katavi wameungana na Wafanyakazi wenzao kote Nchini na Duniani kwa Ujumla kuadhimisha Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani Mei mosi.
Mgeni Rasmi katika maadhimisho hayo,Mkuu wa Wilaya ya Mlele Mh.Filberto Sanga kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mh.Mwanamvua Mrindoko ameongoza Wafanyakazi katika kusherehekea Siku hiyo muhimu ya Wafanyakazi.
Akizungumza katika maadhimisho hayo Mh.Sanga ametoa wito kwa Wafanyakazi Mkoani Katavi kuongeza bidii katika kutekeleza majukumu yao kikamilifu pamoja na kuzingatia Sheria kanuni na Taratibu za Ajira ili kuliletea Taifa maendeleo.
Ameeleza kuwa Serikali inatambua mchango mkubwa wa Wafanyakazi katika Sekta mbalimbali Nchini na kwamba itaendelea kuhakikisha kuwa inasimamia na kulinda maslahi mapana ya Wafanyakazi pamoja na kuboresha stahiki mbalimbali kwa wafanyakazi ili waweze kuleta tija iliyokusudiwa.
Mh.Sanga amewataka Watumishi wa Umma ambao wamekabidhiwa dhamana kubwa ya kutoa huduma kwa Wananchi kujihadhari na tabia na vitendo mbalimbali vinavyoshusha hadhi ya Watumishi wa Umma jambo linaloichafua Serikali.
Amezitaja tabia hizo kuwa ni pamoja na Lugha chafu wakati wa kuhudumia Wananchi,tabia mbaya ya kuomba rushwa ambapo amesisitiza kuwa Serikali haitosita kuchukua hatua a kinidhamu kwa wale wote watakaobainika kuendeleza vitendo hicyo visivyokubalika katika Jamii.
Awali katika Risala ya Wafanyakazi iliyosomwa na uwakilishi kutoka vyama vya Wafanyakazi Mkoani Katavi imeelezwa kuwa watumishi bado wanakabiliwa na changamotyo mbsalimbali jambo linaloathiri kwa sehemu kubwa Utendaji kazi kwa watumishi wa Umma
Aidha wafanyakazi wameiomba serikali kuborsha kuendelea kuboresha maslahi mbalimbali kusudi kuleta tija katika utumishi wa Umma.
Katika Maadhimisho hayo yanayofanyika kila Mwaka Mh.Sanga kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mh.Mwanamvua Hozza Mrindoko amekabidhi Zawadi mbalimbali kwa Wafanyakazi kutoka Taasisi mbalimbali za Umma na Binafsi ili kuamsha ari kwa Wafanyakazi
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved