MKOA wa Katavi umeongoza katika kutekeleza kwa ufanisimasuala ya uwezeshaji wananchi kiuchumi nchini. Mkoa wa pili ni Kigoma na mkoawa tatu ni Pwani ambayo ndiyo imefanya vizuri katika kuhakikisha imesaidiakatika kuwasaidia wananchi kiuchumi nchini.
Washindi hao walikabidhiwa tuzo hizo na mgenirasmi, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati wa Kongamano la Tatu la UwezeshajiWananchi Kiuchumi Katika tuzo hizo, wizara, taasisi na idara za serikalizilizofanya vizuri ni Wakala wa Taifa wa Barabara (Tanroads), mshindi wa pilini Wizara ya Kilimo na Wizara ya tatu ni Wizara ya Maliasili na Utalii.
Taasisi zilizofanya vizuri miongoni mwamifuko ya uwezeshaji nchini ni Shirika Binafsi la Kilimo la Sekta ya KusaidiaWananchi (PASS), Mfuko wa Misitu Tanzania na Mfuko wa Rais wa Uwezeshaji.Katika sekta binafsi washindi ni Kampuni ya Coca-Cola Kwanza Limited, Kampuniya Accacia na kampuni ya Saruji Mbeya.
Katika kundi la mjasiriamali wa mwaka,washindi walikuwa ni Nambuli Agriculture Co Ltd, Ibra Contractor Ltd na MustRead. Katika kapuni zilizojizatiti katika kuandaa biashara, washindi ni UongoziInstitute, Financial Deepining Sector Trust na CND Smith Trust. Akizungumziatuzo hizo, Waziri Mkuu Majaliwa alisema kangamano hilo limetoa tuzo kwa taasisizilizotekeleza vizuri zaidi masuala ya uwezeshaji.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved