Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mhe. Jamila Yusuph amemuakilisha Mhe. Mwanamvua Mrindoko Mkuu wa Mkoa wa Katavi Katika maadhimisho ya miaka 63 ya Uhuru.
Pia amewaongoza Watumishi wa taasisi za Serikali na binafsi, Wanafunzi na Wananchi wa Mkoa wa Katavi kupanda miti katika shule ya msingi Mkapa iliyopo mtaa wa Rungwa Kata ya Kazima kuelekea maadhimisho ya kilele cha miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara ambayo huadhimishwa kila mwaka tarehe 9 Disemba.
DC Jamila amesema mkoa wa Katavi unatekeleza kwa vitendo maelekezo ya Mhe. Rais ya kutaka maadhimisho haya yafanyike kwa kufanya shughuli za kijamii ambapo mkoa wa Katavi umeendelea kupanda miti kwa ajili ya kuimarisha ushirikishwaji wa wananchi.
Shughuli ya upandaji Miti imefanyika katika Shule ya msingi Mkapa na katika barabara ya kuelekea Hospitali ya rufaa ya mkoa Katavi.
Aidha, DC Jamila Yusuph amewaalika wananchi wote wa mkoa wa Katavi kushiriki katika mdahalo kuadhimisha kilele cha sherehe hizo zitakazofanyika katika ukumbi wa Manispaa, Mpanda Social Hall.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved