Pichani:Wananchi mbalimbali wakipewa Elimu kuhusu ufugaji wa Kisasa wa Samaki katika Mabwawa katika banda la Maonyesho la Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika katika Viwanja vya John Makangare yanayoendelea Jijijini Mbeya.
Mkoa wa Katavi ni miongoni mwa mikoa 7 ya Nyanda za Juu kusini inayoshiriki kikamilifu katika maonyesho ya bidhaa za Kilimo Nanenane yanayoendelea katika Viwanja vya John Mwakangare Jijijini Mbeya.
Maonyesho hayo yaliyozinduliwa rasmi 1 Agosti 2022 na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Philip Isdor Mpango yanaendelea kuupamba mji wa Mbeya ikiwa ni Siku ya tatu tangu kuzinduliwa kwake.
Jumla ya Halmashauri tano za Mkoa wa Katavi ambazo ni Manispaa ya Mpanda,Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika,Mpimbwe,Mlele na Nsimbo zinashiriki kikamilifu katika maonyesho hayo ambapo Wajasiriamali wasindikaji wa bidhaa mbalimbali,Wafugaji na Wakulima wamepata fursa ya kushiriki katika maonyesho hayo kwa ajili ya kuonyesha bidhaa mbalimbali zinazozalishwa katika Mkoa wa Katavi.
Onesmo Buswelu Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi amesema maonyesho hayo yanatoa fursa kwa Wakulima,Wafugaji na Wajasiriamali kuonyesha bidhaa mbalimbali zinazozalishwa kutoka katika Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika ambapo ametoa Rai kwa Wananchi mbalimbali kutembelea Banda la Maonyesho la Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika kwa ajili ya kujifunza mbinu bora na za kisasa za Kilimo cha Mazao mbalimbali pamoja na kujifunza shughuli mbalimbali za ufugaji pamoja na Ujasiriamali wa bidhaa mbalimbali
Abdala Kakoso Mjasiriamali na mfugaji Nyuki kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika amewataka Wananchi kufika katika Banda la Halmashauri ya WilayaTanganyika kujionea mazao mbalimbali ya Nyuki pamoja na kujifunza faida mbalimbali zitokanazo na mazao ya Nyuki.
Naye Mstahiki Mea wa Manispaa ya Mpanda Mhe.Haidary Sumry ameeleza kuwa kama Manispaa ya Mpanda imejipanga kuhakikisha kuwa inashiriki kikamailifu katika manyesho hayo huku akiahidi kuwa Mansipaa hiyo itaibuka Mshindi katika Maonyesho hayo ya Nanenane Kikanda Mkoani Mbeya.
Mfugaji wa N,gombe wa Kisasa Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi Bw.Jamal Nasor Mahmoud amesema ni muhimu kwa Wananchi wanaoshiriki katika maonyesho hayo ya Bidhaa za Kilimo nanenane kujifunza zaidi kuhusu ufugaji wa Kisasa wa N,gombe katika banda la Manispaa ya Mpanda na kuachana na N,gombe wa kienyeji kwa kuwa ngombe wa kisasa wana faida kubwa ukilinganisha na ngombe wa Kienyeji ambao kwa wakati huu hawana tija.
Maonyesho ya bidhaa za Kilimo nanenane yataendelea hadi siku ya Kilele chake Tarehe 8 Agosti 2022 ambapo Mgeni rasmi katika Kilele cha Maonyesho hayom anatarajiwa kuwa Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan,Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved