• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Katavi Regional Website
Katavi Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Katavi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Maono na Dhamira
  • Huduma
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na bRasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Halmashauri
      • Miundombinu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • maji
      • Afya
      • Elimu
    • Vitengo
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Idara ya Fedha na Uhasibu
      • Manunuzi
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
    • Muundo wa Taasisi
  • Machapisho
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Videos
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Wilaya
    • Mpanda
    • Mlele
    • Tanganyika
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Livestock
    • Industry and Fishing
    • Minerals
    • Fishing
  • Utalii
    • Katavi National Park
    • Nkondwe Waterfalls
  • Biashara

Kampeni ya Chanjo ya Matone ya POLIO yazinduliwa Mpanda, Mganga Mkuu wa Mkoa awataka Wananchi kutoa ushirikiano kwa timu za Wataalamu.

Posted on: May 19th, 2022

Na: John Mganga-IO Katavi RS

Kampeni ya Utoaji wa Chanjo ya Matone ya POLIO Kwa watoto wenye umri chini ya miaka 5 imezinduliwa rasmi Mkoani Katavi ikiwa ni utekelezaji wa Ratiba ya Kampeni ya Zoezi hilo Kitaifa

Katika Mkoa wa Katavi Kampeni hiyo inatekelezwa katika Wilaya za Mpanda,Mlele,Mpimbwe na Tanganyika ambapo uratibu wa Utoaji wa Matone ya Chanjo ya POLIO umeanza kutekelezwa katika ngazi za Halmashauri zote ndani ya ilaya hizo.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Katavi amezindua Kampeni hiyo kwa kushiriki kutoa chanjo ya Matone ya POLIO ambapo pia amepita baadhi ya nyumba na kutoa chanjo kwa watoto chini ya miaka 5 walioko majumbani katika baadhi ya Nyumba katika Kata ya Ilembo.

Akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Kampeni hiyo katika Kituo cha Afya Ilembo kilichopo Manispaa ya Mpanda, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt.Omari Sukari ametoa rai kwa Wazazi,Walezi na Wananchi kwa Ujumla kutoa Ushirikiano kwa Timu za Wataalamu zinazopita nyumba kwa nyumba kutoa huduma hiyo ya Matone ya  Chanjo ya POLIO.

Amesema lengo la Mkoa ni kuhakikisha kuwa watoto wote wenye Umri chini ya Miaka 5 wanafikiwa na huduma hiyo na kwamba wamejipanga kuhakikisha kuwa maeneo yote yenye watoto kama vile Mashuleni,pamoja na vituo vya Malezi yanafikiwa.

Mganga Mkuu wa Mkoa ametoa wito  kwa Wananchi kupuuza Taarifa zote za Upotoshwaji zinazotolewa na watu wasio na nia njema na badala yake waelekeze maswali ya Ufahamu kwa wataalamu wa Afya wanaopita katika maeneo mbalimbali ili kutoa huduma ya Chanjo hiyo.

Kwa Upande wao Wazazi na walezi waliojitokeza katika kituo cha Afya Ilembo waliowaleta watoto wao wameishikuru Serikali kwa namna ambavyo imechukua hatua za Haraka za kuwakinga watoto na hatari ya Ugonjwa wa POLIO.

Mnamo 13 Mei 2022,Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Mrindoko katika mkutano na Vyombo vya Habari alisema ni muhimu kwa Wananchi kwa Wananchi kutoa Ushirikiano katika kufanikisha utekelzaji wa Kampeni ya utoaji wa Chanjo ya Matone ya POLIO kwa watoto wote wenye umri chini ya miaka 5 ili kufikia azma ya Mkoa ya kuwachanja watoto 189,465.

Kampeni ya Utoaji  wa Chanjo ya Matone ya POLIO kwa watoto wenye Umri chini ya miaka 05 itadumu kwa muda wa siku nne baada ya kuanza 18 Mei 2022 ambapo inatarajia kumalizika ifikapo 21 Mei 2022.

 

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI DESEMBA 2024 December 12, 2024
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA 2025 December 16, 2024
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 04, 2025
  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 January 04, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RC MRINDOKO AZINDUA MAADHIMISHO YA JUMA LA ELIMU (GAWE) 2025

    May 05, 2025
  • RC MRINDOKO AIHAKIKISHIA TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI USALAMA WA UCHAGUZI MKOANI KATAVI.

    April 29, 2025
  • WAZIRI NDEJEMBI AONGOZA MIKAKATI YA KUTATUA MGOGORO WA ARDHI ENEO LA WESTERN, KITONGOJI CHA LUHAFWE – H/ WILAYA YA TANGANYIKA

    April 24, 2025
  • PPPC WATOA ELIMU UIBUAJI WA MIRADI INAYOTEKELEZWA KWA UBIA.

    April 03, 2025
  • Tazama Zote

Video

UZINDUZI RATIBA YA SAFARI ZA NDEGE ATCL SIKU YA JUMATATU 23 MEI 2022
Video zinginezo

Wavuti wa Haraka

  • SALARY SLIP PORTAL
  • FURSA ZA UTALII KATUMA MKOANI KATAVI
  • KATAVI RS HABARI
  • KATAVI RS HABARI YOUTUBE

Wavuti mwambata

  • Mpanda Municipal Council
  • Mpimbwe District Council
  • Mpanda District Council
  • Nsimbo District Council
  • Mlele District Council
  • Tovuti ya utumishi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani

Wasiliana nasi

    Mpanda-Katavi (Mkoani Area)

    Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi

    simu: 025-2957108

    Mobile:

    Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera za Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • ramani
    • Huduma

Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved