Pichani:Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Mrindoko akimtunuku cheti cha Mshindi wa kwanza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Bi.Theresia Irafay kwa kuibuka kidedea katika ukusanyaji wa mapato Mwaka wa fedha 2021/2022 katikaUkumbi wa Maji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika ulioko Manispaa ya Mpanda.
Mpanda.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Mrindoko amezipongeza Halmashauri na Taasisi mbalimbali mkoani humo kwa kufanikisha Mkoa huo kufikia na kuvuka malengo ya ukusanyaji wa mapato kwa mwaka wa fedha 2021/2022.
Mhe.Mrindoko ametoa pongezi hizo 16 Agosti 2022 katika kikao cha Tahmini ya utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Mkoa kilichokutanisha Taasisi mbalimbali za Serikali Mkoani humo kwa lengo la kutathmini utekeleaji wa Mpango na Bajeti kwa mwaka wa fedha 2021/2022 katika ukumbi wa Maji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika.
Mhe.Mrindoko amezitaka Halmashauri Mkoani Katavi pamoja na Taasisi mbalimbali zinazohusika katika ukusanyaji wa mapato ya Serikali kutobweteka kwa pongezi na badala yake kuongeza juhudi zaidi za ukusanyaji wa mapato kwa mwaka wa fedha 2022/2023.
Akiwasilisha Taarifa ya tahmini ya mapato ya ndani ya Halmashauri kimkoa Katibu tawala msaidizi sehemu ya usimamizi wa Serikali za Mitaa Bw.Florence Crisant ameeleza kuwa hadi kufikia 30 Juni 2022 Halmashauri za Mkoa wa Katavi kwa mwaka wa fedha 2021/2022 zilikuwa zimekusanya jumla ya Shilingi Bilioni 13.6 sawa na Asilimia 112 ya Makisio ya shillingi Bilioni 12.1.
Taarifa hiyo imezitaja Halmashauri 3 kati ya 5 za Mkoa wa Katavi kuvuka Malengo ya ukusanyaji ikiongozwa na Halmashauri ya Wilaya ya Mlele ambayo imekusanya shilingi 1, 774,087,421 sawa na Asilimia 185 ikivuka lengo lake la mwaka la makusanyo ya Shilingi 957,000,000 katika mwaka wa fedha 2021/2022.
Halmashauri zingine zilizovuka malengo ya ukusanyaji wa mapato ni pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe ambayo imefanikiwa kuvuka lengo la makusanyanyo ya mwaka ya Shilingi 1,973,554,176 kwa kukusanya Shilingi 2,540,837,091 sawa na asilimia 129 ikishika nafasi ya Pili huku Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo ikivuka malengo ya mwaka wa fedha 2021/2022 ya Shilingi 1,191,000,000 na kukusanya Shilingi 1,421,815,380 ikishika nafasi ya tatu.
Aidha Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika imeshika nafasi ya nne ikitembea ndani ya makisio yake kwa kukusanya Shilingi 4,452,617,530 sawa na Asilimia 100 ikifuatiwa na Manispaa ya Mpanda nafasi ya tano ambayo imekusanya Asilimia 97 ya Makisio ya Shilingi 3,577,000,000.
Aidha katika Kikao hicho Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Mkoani Katavi pia katika Taarifa yake ilionyesha kuvuka lengo kwa ongezeko la Asilimia 32 kwa kukusanya zaidi ya Shilingi Bilioni 8 kwa mwaka wa fedha 2021/2022.
Kwa upande wa Sekta ya Madini Ofisi ya Afisa Madini Mkazi katika taarifa yake ilionyesha kuvuka malengo ya ukusanyaji kwa kukusanya Shilingi 6, 256, 198, 091.67 sawa na Asilimia 131.71 ukilinganisha na lengo la mwaka la makusanyo ya Shilingi Bil.4.75.
Picha 2.Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Mrindoko akimtunuku Cheti Bi.Catherine Mashalla,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe kwa kuibuka mshindi wa pili katika ukusanyaji wa Mapato Kimkoa 16 Agosti 2022 katika ukumbi wa Maji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganhyika ulioko Manispaa ya Mpanda.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Mrindoko akimtunuku cheti Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Bw.Mohamed Ramadhani kwa kuibuka Mshindi wa tatu kimkoa katika ukusanyaji wa mapato.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi akimtunuku cheti Meneja wa TRA mkoa wa Katavi.Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Mkoa wa Katavi nao ni miongoni mwa Taasisi zilizovuka malengo ya ukusanyaji wa Mapato Mkoani Katavi
Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Katavi akitunukiwa zawadi ya cheti kutoka kwa mkuu wa Mkoa wa Katavi kwa kuvuka mlengo ya ukusanyaji wa Mapato.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved