Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mh.Mwanamvua Mrindoko alipozungumza na Waandishi wa Habari 13 Mei 2022 Ofisini kwake
Na:John Mganga-IO Katavi RS
Watoto wapatao 189,465 chini ya Miaka 5 wanatarajiwa kupata chanjo ya Ugonjwa wa Polio Mkoani Katavi ikiwa ni jiitihada za Serikali kuchukua tahadhari kufuatia tishio la mlipuko wa Ugonjwa huo baada ya Visa kadhaa vya watoto kukutwa na maambukizi ya Polio kuripotiwa katika Nchi jirani ya Malawi.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mh.Mwanamvua Mrindoko alipozungumza na Waandishi wa Habari 13 Mei 2022 Ofisini kwake ambapo ameeleza kuwa chanjo hiyo itatolewa rasmi kuanzia Tarehe 18 hadi Tarehe 21 Mwezi Mei 2022.
Mhe. Mrindoko ameeleza kuwa awali Serikali iliahirisha zoezi la utoaji wa chanjo ya Polio ili kuweka sawa maandalizi kusudi zoezi hilo la utoaji wa chanjo liweze kutolewa kwa ufanisi zaidi kama ilivyokusudiwa.
Ameeleza kuwa Zoezi hilo litatekelezwa na Wataalamu wa Afya kwa kupita nyumba kwa nyumba ambapo watatoa chanjo hiyo ya matone kwa njia ya mdomo na pia katika maeneo yote ambayo watoto watapatikana.
Aidha Mh.Mrindoko amewahakikishia Wananchi wote kuwa Chanjo ya Polio inayotolewa ni salama na haina madhara yeyote na kwamba kwa wale wote wenye maswali wanapaswa kuwauliza wataalamu wa Afya waliopo katika maeneo mbalimbali katika Vituo vya kutolea hduma za Afya.
Amekemea vikali tabia ya Wananchi wanaopotosha Taarifa mbalimbali kuhusu Chanjo ambapo ameeleza kuwa serikali haitosita kuchukua hatua za kinidhamu kwa wale wote watakaobainika kupotosha Taarifa za Chanjo.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved