BARABARA ZABORESHA UCHUKUZI NA USAFIRISHAJI BIDHAA NA ABIRIA MKOANI KATAVI
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Mwanamvua Mrindoko amesema uchukuzi wa bidhaa na usafirishaji wa abiria umerahisishwa kwa wananchi ndani na nje ya Mkoa wa Katavi kutokana na uwekezaji mkubwa unaoendelea kufanyika katika sekta ya miundombinu ya barabara katika mkoa huo.
Mhe. Mrindoko ameyasema hayo katika kikao cha Bodi ya Barabara kilichofanyika leo kwenye ukumbi wa Manispaa ya Mpanda uliopo Mjini Mpanda
Amesema Serikali yetu imeendelea kujenga barabara vijijini, kukarabati barabara na kukamilisha barabara mbali mbali, hivyo kuweka mazingira rahisi ya barabara kupitika muda wote kwa mwaka.
Mhe. Mrindoko amezitaja barabara za Vikonge na Stalike, Barabara za Mjini Mpanda, Barabara ya Mpanda-Tabora kuwa ujenzi wake umekamilika na kurahisisha uchukuzi wa bidha na usafirishaji wa abiria, hivyo kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi wa ndani na nje ya Mkoa wa Katavi.
Amesema ujenzi wa miradi mingine ya barabara unaendelea pia katika maeneo mbali mbali ya mkoa mfano Kibaoni-Stalike na Vikonge-Luhafe-Kigoma.
Hata hivyo kiongozi wa mkoa huyo amesikitishwa na vitendo vya wizi na uharibifu wa miundombinu ya barabara unaofanywa na baadhi ya wananchi wasiowaaminifu wanaoiba taa na nguzo za taa za barabarani.
Kufuatia uharibifu huo, Mhe. Mrindoko ameliagiza Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi kuwakamata watu wote wanaojihusisha na wizi huo na kuwachukulia hatua za kisheria ili kukomesha tabia ya uharibifu ya miundombinu ya barabara.
Pamoja na juhudi zinazofanywa na Jeshi la Polisi mkoani Katavi, Mhe. Mrindoko amewataka pia wananchi wote wa Mkoa wa Katavi kulinda na kutunza miundombinui ya barabara ili iweze kuwanufaisha wananchi wa kizazi hiki na kijacho.
Umbali (kwa kilomita) wa mtandao wa barabara za umma za kitaifa na wilayani na vijijini umeendelea kuongezeka kila mwaka kutokana na uwekezaji mkubwa unaofanywa na serikali katika miundombinu ya barabara na madaraja nchini.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved