Pichani:Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Mrindoko alipukutana na kuzungumza na Viongozi wa Asasi zisizo za kiserikali 12 Septemba katika ukumbi wa Manispaa ya Mpanda
Mpanda -Katavi.
MKUU wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko, amezitaka asasi zisizo za kiserikali (NGO), zisitumike kuharibu maadili na tamaduni za kitanzania, demokrasia, amani na uhuru wa nchi.
Mrindoko ameyasema hayo 12 Septemba 2022 katika kikao kilichokutanisha mashirika hayo, kilicholenga kujadili changamoto na maendeleo ya Mkoa wa Katavi, kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Mpanda ambapo amezisisitiza asasi hizo kuepuka kutumika kisiasa na kuharibu maadili ya Kitanzania
Pia amezitaka taasisi hizo kushirikiana na serikali katika mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili katika mkoa huo, ikiwemo ubakaji, ulawiti na mimba za utotoni.
“Mkoa wetu wa Katavi matatizo hayo yanaendelea kutufedhehesha, masuala ya ubakaji na ulawiti yanaendelea kuongezeka, mimba na ndoa za utotoni, utoro shuleni, ajira za watoto, kazi za kingono, bado hamjaweza kufanya kazi zenu vizuri, hatujaona kama NGO zinazogusa maeneo hayo zinafanya kazi ya kutosha,” amesema na kuongeza:
“Mtoke na mkakati tunamalizaje suala hilo, suala hili si wajibu wa serikali peke yake na mashirika, hapa mmetaja kwamba mnayafanya masuala hayo, lakini kwa kweli bado yapo na yanaendelea kuongezeka na NGO mpo, shughuli zenu zinagusa hapo, je mnafanya wapi mambo haya mbona hatuoni matokeo? Amehoji RC Mrindoko.
Ameonya kuwa hatavumilia asasi yoyote, ambayo itabainika kuwa na lengo la kuchochea au kuhamasisha mapenzi ya jinsia moja na endapo itabainika hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Nae ofisa maendeleo ya jamii Mkoa wa Katavi Willison Kennedy, amesema changamoto inayofanya mkoa huo kushindwa kutatua baadhi ya matatizo ni kutokana na kuwa na mashirika machache ya kimataifa, ambayo yanapokea ruzuku kutoka nje, huku akidai kuwa mashirika madogo yaliyopo ndani ya mkoa mengi hukosa ruzuku, kwa ajili ya kutelekeza miradi mbalimbali.
Mashirika hayo yamekutana kujadili mambo mbalimbali yanayo endelea katika Mkoa wa Katavi, kisha kutoka na ripoti ya pamoja na kwenda kuwasilisha katika mkutano wa kitaifa.
MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved