Friday 6th, December 2024
@HLMASHAURI YA WILAYA YA TANGIKA /SM KASEKESE
Mkoa wa Katavi Sikuya Tarehe 1 Desemba 2022 utaungana na mikoa mingine kote Nchini kuadhimisha siku ya UKIMWI Duniani katika Uwanja wa Shule ya Msingi Kasekese ulioko Wilayani Tanganyika.
Katika maadhimisho hayo ya siku ya UKIMWI Duniani kimkoa Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Hoza Mrindoko atakua Mgeni rasmi.
Maadhimisho hayo yataambatana na shughuli mbalimbali zikiwemo upimaji wa VVU na utoaji ushauri nasaha,utoaji wa elimu ya magonjwa yasiyoambukiza pamoja na Elimu ya Lishe.
Aidha,itakuwepo pia huduma ya uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake,uchunguzi wa Ugonjwa wa Kifua kikuu,pamoja na elimu ya uzazi wa mpango ambapo huduma hizo zitatolewa bila malipo yoyote.
Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani inasema, Imarisha Usawa.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved