
Serikali inaendelea na ujenzi wa Bandari ya Karema, iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika, Kata ya Karema, Kijiji cha Karema, kwa gharama ya zaidi ya Shilingi Bilioni 47.9.
Mradi huu unalenga kuboresha usafiri wa majini katika Ziwa Tanganyika, kurahisisha usafirishaji wa abiria na mizigo, pamoja na kuchochea biashara na maendeleo ya kiuchumi katika Mkoa wa Katavi na kanda ya magharibi kwa ujumla.
">

Serikali imekamilisha ujenzi wa jengo jipya la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Mpanda, mkoani Katavi, kwa gharama ya zaidi ya Shilingi Bilioni 1.4.
Uwanja huo unahudumiwa na Shirika la Ndege la ATCL mara tatu kwa wiki, ambapo kila safari hubeba abiria wapatao 76. Kukamilika kwa jengo hili kunaboresha huduma za usafiri wa anga na kuchochea maendeleo ya kiuchumi katika mkoa wa Katavi.
">

Serikali imekamilisha ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi, iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda, Kata ya Kazima, Mtaa wa Rungwa, kwa gharama ya zaidi ya Shilingi Bilioni 18.3.
Hospitali hiyo tayari imeanza kutoa huduma kwa wananchi na imekuwa msaada mkubwa katika kuboresha huduma za afya mkoani Katavi, pamoja na kupunguza rufaa za wagonjwa kwenda mikoa ya jirani.
">